Tulishatuma usajili wetu TFF- Yanga

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Uongozi wa Yanga umethibitisha kwamba ulishawasilisha usajili wake ndani ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF na wanashangaa wanapoambiwa kwamba wamekaidi.

Yanga ilishatuma usajili wake mapema kwenye mfumo wa TMS, Ila kwa siku za karibuni kulikuwa na matatizo ya mtandao ambapo kuna muda taarifa zilionesha usajili huo kuonekana na kutoonekana!ndipo Yanga SC walipowasiliana na wahusika waliambiwa ni matatizo ya mtandao. . Jumamosi ilikuwa siku ya mwisho na ndio siku tulikuwa na mkutano mkuu wa dharula, makamu mwenyekiti Clement Sanga aliwasiliana na katibu mkuu Baraka Deusdedit ambaye alithibitisha kuwa yametumwa!

Leo sekretarieti ya Yanga itakaa na TFF kutolea ufafanuzi wa jambo hilo. . Tuwe na subira wala tusilaumiane tusubiri mrejesho wa maafikiano ya kikao hicho.