Tambwe, Ngoma waitisha African Lyon

Na Saida Salum

Washambuliajj wawili wa kimataifa wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Amissi Tambwe raia wa Burundi na Donald Ngoma raia wa Zimbabwe  wameanza kuipasua kichwa timu ya African Lyon ambayo imepanda Ligi kuu msimu huu.

African Lyon itakutana  na Yanga siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, lakini hofu yao ipo kwa washambuliaji hao hatari wa Yanga.

Kocha wa African Lyon, Myugoslavia Dragan Popadic ambaye pia aliwahi kuinoa Simba mwaka 1993 na kuifikisha fainali ya kombe la CAF, amesema Yanga ina washambuliajj wawili ambao ni hatari na mabeki wake watakuwa na kazi kubwa kuwakabili.

Lakini kocha huyo amesema atawawekea mabeki watulivu na wataweza kuwazuia na hawataweza kuleta madhara langoni kwao, African Lyon iliwalazimisha sare ya 1-1 Azam FC katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jijj la Dar es Salaam