Na Paskal Beatus, Shinyanga
Uongozi wa timu ya Stand United umesema wako mbioni kujitoa Ligi kuu bara baada ya kuchoshwa na mgogoro uliochochewa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) na kuzaa makundi mawili Stand Kampuni na Stand Wananchi.
Stand ambayo tayari imeshacheza mchezo mmoja na Mbao FC ya Mwanza na kuambulia pointi moja, imeweka bayana mpango wake wa kujitoa ili pande zote zinazolumbana zione madhara ya mgogoro na hatimaye timu ishuke daraja.
Uongozi huo ulithibitisha jana ambapo umeonekana kuibebesha lawama TFF kwa kushindwa kuwapatisha na badala yake kuchochea mgogoro uliopelekea kuigawa timu hiyo, endapo Stand itajitoa Ligi kuu bara, itasababisha Ligi hiyo kusimama ili kupisha mabadiliko ya ratiba, na pia huenda timu hiyo ikashushwa daraja hadi ngazi ya wilaya kutokana na kosa la kujitoa