Staa Wetu: Mshamu Hassan "Mfuga Njiwa" Mtangazaji chipukizi wa mpira wa miguu, mwenye ndoto za kumfikia Juma Nkamia
Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Anaitwa Mshamu Hassan lakini anajulikana zajdi kwa jina la Baba Nuraty Mfuga Njiwa, Ni mtangazaji wa redio Sibuka 94.5 FM inayosikika nchi nzima ikiwemo Dar es Salaam.
Mtangazaji huyo ameanza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na utangazaji wake kuvutia wengi na wale waliopata bahati ya kumsikia wamefurahishwa naye.
Alianza kazi hiyo akiwa kama mwanasalamu wa kawaida katika redio mbalimbali kiasi kwamba akajipatia umaarufu, Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Mfuga Njiwa alisema utangazaji ni kazi aliyoipenda ingawa hakupata kujua ataianzia wapi.
Salamu zilimwezesha kupata nafasi ya kujulikana na wengj na ndipo alipoweza kufanya interview katika vituo vya redio 13 na kimoja cha televisheni, Lakini anasema ni redio Sibuka pekee ndiyo iliyotambua kipaji chake.
Akaanza kazi katika redio hiyo na kipindi cha michezo cha kila siku cha Sportaiment na kile cha wiki kinachofanyika kila siku ya Jumamosi kiitwacho MBS ambavyo vyote anashiriki.
Pia Mfuga Njiwa amekuwa akipata nafasi ya kutangaza mpira wa miguu, Mtangazaji huyo ameanza kusikika katika mechi kadhaa za kirafiki na zile za Ligi kuu bara zinazofanyika katika viwanja mbalimbali hapa nchini.
Mfuga Njiwa aliyepata elimu yake ya msingi na sekondari Temeke Dar es Salaam alizaliwa katika hospitali ya Temeke mwaka 1983, baba yake ni mzaliwa wa Mikindani mkoani Mtwara wakati mama yake ni mzaliwa wa Kilwa mkoani Lindi.
Mtangazaji huyo chipukizi ana ndoto kubwa za kumfikia mtangazaji mkongwe Juma Nkamia ambaye kwa sasa ni mbunge, Nkamia alikuwa akitangaza vema mpira wa miguu alipokuwa katika redio ya TBC Taifa.
Kwa wale waliobahatika kumsikia wanakiri kabjsa kuwa Mfuga Njiwa ni Nkamia wa pilj kwani ana kasi kubwa anapotangaza na akionekana kama mzoefu, aidha mtangazaji huyo huwa sambamba na wenzake David Pasko, John Ndeki, Salama Ngale, Omary Juma na mwingine anayefahamika kwa jina la Promise