Simba yatakata Taifa, yaifumua AFC Leopards 4-0

Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM

SIMBA SC jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam imeifanyia kitu mbaya AFC Leopards baada ya kuifumua mabao 4-0 mchezo wa kirafiki wa kimataifa kuadhimisha Simba Day.

Simba inayonolewa na Mcameroon Joseph Marius Omog iliingia uwanjani kwa kasi ikiliandama lango la Leopards, Ibrahim Ajibu Migomba alitangulia kuipatia bao la kwanza timu yake lilikifungwa kipindi cha kwanza.

Hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao la kwanza, kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo vijana wa Simba waliweza kuongeza mabao mengine matatu, Ajibu aliongeza bao lingine la pili kabla ya Shiza Kichuya kuongeza bao la tatu.

Wakicheza mbele ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Poul Makonda, vijana wa Simba waliongeza bao la nne lililofungwa na Laudit Mavugo raia wa Burundi, hadi mpira unamalizika Simba 4 AFC Leopards 0