Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
SIMBA SC jioni ya leo imebanwa mbavu na JKT Ruvu katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa kutoka suluhu 0-0 mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi nne ikiwa imecheza mechi mbili wakati JKT Ruvu imecheza mechi moja na siku ya Jumatatu inaumana na Yanga katika uwanja huo huo wa Taifa.
Simba wakiwa na washambuliajj wake Fredrick Blagnon na Laudit Mavugo walionekana kulishambulia lango la JKT Ruvu lakini ngome ya JKT ilikuwa imara na kuzuia hatari hizo, hata hivyo Blagnon na Mavugo hawakuwa katika maelewano mazuri kwani walikosa mabao kadhaa.
Kipindi cha pili Simba walimtoa Blagnon na kumwingiza Ibrahim Ajibu 'Kadabla' lakini naye hakuweza kubadilisha mchezo, kipa wa JKT Ruvu Said Kipao anastahili pongezi kwa kuiokoa timu yake isifungwe katika mchezo huo