Simba yamleta Mavugo

Na Prince Hoza, Dar es Salaam

BAADA ya bilionea Mohamed Gulam Dewji 'Mo' kuimwagia mamilioni, Klabu ya Simba imefanikiwa kumleta nchini mshambuliaji wa Vital'0 ya Burundi, Laudit Mavugo tayari kabisa kwa kujiunga nao.

Mavugo alipokelewa na mashabiki wa Simba kwenye uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere na alikabidhiwa jezi ya Simba yenye namba 45, kutua kwa mshambuliaji huyo aliyekuwa gumzo kwa muda mrefu kunafufua matumaini ya Wekundu hao katika kurejea kwenye makali yake.

Mavugo anatarajia kusaini mkataba wa miaka miwili hivi karibuni na atatambulishwa kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kuadhimisha Simba Day dhidi ya Interclube Agosti 8 mwaka huu