Simba na Ndanda kesho Taifa

Na Prince Hoza

Simba SC kesho jioni itajitupa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwakaribisha "Wana kuchele" Ndanda FC mchezo wa ufunguzi Ligi kuu ya Vodacom Tanzanis bara.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na matumaini kibao hasa baada ya kutoka kucheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa ambapo moja iliwafunga AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 na nyingine ikatoka sare ya 1-1 na URA ya Uganda.

Wekundu hao pia wanaingia uwanjani wakiwa na furaha na kikosi chao kilichosheheni nyota kama Laudit Mavugo, Method Mwanjali na Fredrick Blagnon, Lakini Ndanda hawatishiki na majina kwani wao nao wanaye Salum Telela 'Abo Master' aliyetokea Yanga SC hivyo wametamba kutoa upinzani mkali katika mchezo huo, Mwamuzi wa yote ni dakika tisini