Simba kuivaa URA J,pili

Na Prince Hoza

Baada ya Jumatatu iliyopita kuipa kipigo kitakatifu AFC Leopards ya Kenya cha mabao 4-0, Kikosi cha Simba SC kinatelemka tena uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuwavaa URA ya Uganda mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Vijana wa Simba walicheza kandanda safi siku ya Jumatatu waliyosheherekea Simba Day ikiadhimisha siku yake ya kuzaliwa iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0, magoli ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajibu (Mawili), Shiza Kichuya na Laudit Mavugo.

Mashabiki wa Yanga wamekibeza kikosi cha Leopards wakidai ni dhaifu na ndio maana Simba kashinda mabao mengi hivyo URA inakuja kutoa ushindani kwa mianba hiyo, Leopards wanashika nafasi ya 12 ikiwa mkiani, lakini URA imekuwa ikiisumbuaga sana Simba hivyo Jumapili na mwisho wa ubishi