Simba balaa sana yaiua Ndanda 3-1

Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam

SIMBA SC jioni ya leo imeichapa Ndanda FC mabao 3-1 na kujikusanyia pointi tatu muhimu katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Vijana wa Simba wakiwa na hamasa kubwa kutoka kwa mfanyabiashara Mohamed Gulam Dewji "Mo Dewji", walianza kuliandama lango la Ndanda na kujipatia bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji wake mpya raia wa Burundi, Laudit Mavugo.

Bao hilo la Mavugo limeingia kwenye rwkodi ya kuwa bao la kwanza msimu huu kwenye uwanja huo, Ndanda wakasawazisha kupitia kwa Omari Mponda na kufanya timu hizo ziende kupumzika zikiwa sare.

Kipindi cha pili Simba walimtoa mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu na kuingia Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast, mabadiliko hayo yakazaa matunda kwani Simba ilipata bao la pili lililofungwa na Blagnon.

Shiza Ramadhan Kichuya akafunga bao la tatu na la ushindi, kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi tatu na huenda ikawa kileleni mwa msimamo wa ligi, mbali na rwkodi ya Mavugo, Simba imeandika rwkodi nyingine kwa wachezaji wake wapya kufunga katika mchezo huo