Na Mwandishi Wetu
Mshambuliajj wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga KRC Genk inayoshiriki Ligi kuu nchini Ubelgiji Mbwana Ali Samatta anaongoza kwa upachikaji magolj kwenye ligi ya nchi hiyo.
Samatta amefunga magoli manne wakati anayemfuatia amefunga magoli matatu, kung' ara kwa mshambuliajj huyo wa zamani wa African Lyon, Simba SC na TP Mazembe kunatokana na juhudi zake binafsi ambako kutamfanya apate soko haraka.
Samatta alijiunga na Genk mwanzoni mwa mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DR Congo aliyoipa ubingwa wa Afrika, Samatta ndiye mwanasoka bora wa bara la Afrika kwa mwaka huu