Mshambulizi nyota raia wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kung' ara katika timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji baada ya kuifungia bao muhimu wakati timu yake ikiifunga Locomotive mabao 2-0 na kutinga kwenye hatua ya makundi kombe la Ulaya.
Samatta alitangulia kufunga bao la kwanza katika dakika ya pili ya mchezo kipindi cha kwanza kabla ya Leon Beila kuongeza la pili, kwa maana hiyo Genk imefuzu kwenye makundi na inaweza kujikuta inapangwa pamoja na Man United inayonolewa na kocha mbwatukaji Jose Mourinho.
Tangu ajiunge na Genk, Samatta amekuwa na mwanzo mzuri akifanikiwa kufunga kila mechi, mshambuliaji huyo wa zamani wa Tp Mazembe anaongoza kwa ufungaji katika ligi kuu ya nchi hiyo