Rage kumburuza mahakamani Hanspoppe

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage amemtaka mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Zacharia Hanspoppe kumuomba radhi ndani ya siku aaba ama sivyo atamfikisha mahakamani kutokana na kauli yake aliyoitoa jana ikisema Rage aliwahi kuhamishia fedha za usajili wa Mbwana Samatta kwenye akaunti ya mkewe.

Akizungumza leo na kipindi cha michezo cha redio Efm, Rage amemtaka Zacharia Hanspoppe kumuomba radhi haraka kabla hajachukua maamuzi ya kwenda kumfungulia mashitaka mahakamani, 'Tayari nimeshaongea na mwnaasheria wangu na sasa nampa siku saba Hanspoppe kuniomba radhi ama sivyo nampandisha kizimbani', alisema Rage.

Jana Hanspoppe akiongea kupitia redio hiyo alisema anawashangaa Takukuru kumkamata Evans Aveva kwa kosa la kuhamisha fedha za klabu ya Simba za usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi wakati Ismail Aden Rage akiwa mwenyekiti wa Simba aliwahi kuhamisha fedha za usajili wa Mbwana Samatta kwenye akaunti ya mkewe