Mzee Yusuph aachana na taarabu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Gwiji la muziki wa taarabu nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa bendi yake ya Jahazi, Mzee Yusuph ametangaza kuachana na muziki huo na kuamua kumrejea mungu.

Taarifa zilizotufikia ambazo zimethibitishwa na yeye mwenyewe zinasema kuwa ameamua kuachana na muziki na kuamua kumrejea mwenyezi mungu.

Yusuph amedai binadamu tuna deni kubwa kwa mwenyezi mungu hivyo umefika wakati wa kumrejea na kuachana na mambo ya duniani, mwanamuziki huyo ameongeza kuwa ataendelea kuwasapoti wanamuziki chipukizi