Mkude ainusuru Simba

Na Prince Hoza, Dar es Salaam

Goli la kusawazisha lililofungwa na Jonas Gerrald Mkude jioni ya leo limeiokoa klabu yake ya Simba baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1 na URA ya Uganda mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

URA ambao juzi waliilazimisha Azam FC kwenye uwanja wao wa Azam Complex Chamazi kwa kufungana 1-1, walikuwa wa kwanza kuandika bao la kwanza kipindi cha kwanza kabla ya Mkude ambaye leo hii ameanza majukumu mapya ya kuwa nahodha wa Simba.

Mkude amechukua nafasi ya Mussa Hassan Mgosi ambaye amestaafu rasmi kucheza soka la ushindani na leo ameaga rasmi, Mgosi sasa anakuwa meneja wa Simba akisaidiana na Abbas Ally.

Vijana wa Simba walicheza kandanda safi na la kupendeza huku mshambuliaji wake mpya Laudit Mavugo akicheza vizuri ingawa hakuwa kwenye kiwango chake kama alichokionyesha katika mchezo uliopita na AFC Leopards