Michano: Mkola Man, Mwanahip hop anayesota, ni sawa na mkulima wa pamba wakati wa njaa hawezi kuzila

Na Ikram Khamees, Dar es Salaam

Yap....yap...yap...Michano yangu ya leo inamchana msanii wa miondoko ya Hip hop mkazi wa Hale mkoani Tanga, huyu jamaa ameanza muziki kitambo ila naye bado hajapata bahati ya kutoka.

Alijaribu kutoka miaka minne iliyopita alipoachia ngoma yake ya kwanza 'Utajiri hewa' lakini haikufanya vizuri, akaachia nyingine 'Mr Mapesa' ambayo ilisumbua kidogo TBC FM hadi kuingia kumi bora.

Mkola Man akaachia nyimbo nyingine kama 'Kilevi changu', 'Malovedavi time', 'Jana na leo' na 'Kitabu cha historia' aliyoiachia sasa, mwanamuziki huyo anajitahidi kutoa nyimbo ila tatizo promo.

Amekuwa akifanya promo ya kitoto kwani zinatamba muda mfupi na kuzimika, Yaani namfananisha Mkola Man na mkulima wa pamba ambaye anajitahidi kutayalisha shamba na kulima lakini soko kamili la biashara hiyo halijui.

Kinapofika kipindi cha njaa anashindwa kula pamba, basi tukutane wiki ijayo Ikram Khamees ndani ya michano