Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Mshambuliajj na nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi ameteuliwa kuwa meneja wa Simba kuanzia leo kuchukua nafasi ya Abbas Seleman aliyepewa cheo kingine cha uratibu.
Kwa maana hiyo Mgosi anastaafu rasmi kucheza soka la ushindani na sasa atakuwa bize katika kazi yake mpya ya umeneja, wakati Simba ikimpa ulaji Mgosi, kiungo mkabaji Jonas Mkude amechaguliwa kuwa nahodha mpya akirithi mikoba ya Mgosi.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Simba, Hajji Manara amethibitisha taarifa hizo, pia Manara amesema, Mchezaji Peter Mwalyanzi amepelekwa kwa mkopo African Lyon inayoshiriki Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara