Manji amaliza mzozo Yanga

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Yanga Yusuff Manji juzi usiku alikutana na wachezaji wa Yanga na kuwalipa malimbikizo ya posho zao zote za msimu uliopita kutokana na kutwaa mataji yote matatu nchini, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Pia Manji alitumia zaidi ya masaa 4 kujadiliana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi, majadiliano hayo yalihusu tathmini ya ushiriki wa Yanga katika michuano mbalimbali msimu uliopita kisha waliweka makubaliano na malengo kwa msimu huu, Manji aliwapa hamasa zaidi kwa kuwaambia wana-Yanga wanahitaji vikombe zaidi msimu huu na wanapaswa kufika mbali katika michuano ya kimataifa.Benchi la ufundi pamoja na wachezaji kwa kauli moja wameahidi kuwapa raha zaidi wanajangwani msimu huu.