Manji akodishwa Yanga miaka 10

Na Ikram Khamees, Dar es Salaam

Wanachama wa klabu ya Yanga mchana wa leo kwa hiari yao wamekubaliana kumkodisha mwenyekiti wao ambaye pia ni Mkurugenzi wa Quality Group, Yusuph Mehbood Manji kwa kipindi cha miaka 10.

Wakikubaliana kwa hiari wanachama hao wameridhia Manji apewe timu hiyo na sasa itakuwa mali yao binafsi, Manji ataiendesha klabu hiyo ambapo amesema atachukua asilimia 75 za mapato ya klabu na asilimia 25 ataziacha kw wanachama.

Pia atabaki na timu pamoja na nembo ya klabu wakati jengo na mali nyinginezo zitasalia kwa wanachama, Manji amedai ataiendesha klabu hiyo na hata kama akipata hasara au faida hawezi kuachana nayo mpaka miaka kumi itimie.

Wakati huo huo Manji amewafuta uanachama Salum Mkemi, Hashim Abdallah na Ayoub Nyenzi, Manji amesema hawezi kufanya nao kazi wanachama hao ambao pia ni wajumbe wa kamati ya utendaji, Manji aliungwa mkono na wanachama wote walioudhuria kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee