Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam
Taarifa zilizosambaa jijini Dar es Salaam ni kujiuzuru kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuph Mehbood Manji (Pichani), Manji amefikia uamuzi hasa baada ya kutoungwa mkono na Wanayanga wenzake katika mpango wake wa kutaka kuikodisha klabu hiyo.
Manji alitaka kuikodisha Yanga kwa muda wa miaka kumi lakini akakumbana na maneno ya kejeli na vitisho kutoka kwa Wanayanga, akizungumza jioni hii mara baada ya kuenea kwa taarifa za kujiuzuru, Manji amesema bado hajawa tayari kuzungumzia taarifa hizo lakini kwa sasa anaomba aachwe kwanza.
Kwa maana hiyo Manji amejiweka kando Yanga hivyo sasa watakuwa katika wakati mgumu, Manji amejikuta akiandamwa na viongozi wa serikali juu ya mpango wake huo, hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Poul Makonda alipost maneno katika ukurasa wake wa Facebook ambao ulionekana kumkashifu bosi huyo wa Yanga ambaye ni mmiliki wa Quality Group