KIUNGO WA YANGA AKWAMA UMANGANI

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Kiungo wa zamani wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC, Abdi Kassim 'Babbi' amekwama kuendelea kuitumikia timu yake ya Ligi kuu nchini Malysia na sasa yupo yupo Zanzibar akihaha kusaka timu ya kujiunga nayo.

Babbi mwenye rekodi ya kufunga bao la kwanza Uwanja wa Taifa Dar es Salaam akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars, alijiunga na timu ya Malysia ambapo mkataba wake umenalizika.

Baada ya kumalizika mkataba wake, Babbi ameshindwa kuendeleza mkataba mwingine hasa baada ya timu hiyo kushindwa kufikia maelewano naye, kiungo huyo amerejea Zanzibar akisaka timu