Kipre Tchetche azitosa Simba, Yanga na Azam, asaini Al Na

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mshambuliaji Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast ametambulishwa na timu ya Al Nahdha ya Oman inayoshiriki Ligi kuu na amezitosa kabisa Yanga na Simba ambazo zilivumisha kutaka kumsajili.

Kipre aliyekuwa anakipiga Azam FC kwa mafanikio makubwa, ameamua kuachana nayo na jana akatambulishwa na uongozi wa timu ya Al Nahdha ya Oman, kwa maana hiyo Mshambuliaji huyo ameondoka rasmi kwenye soka la bongo