Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) usiku wa leo limeidhinisha jina la mlinzi wa kulia wa Yanga, Hassan Khamis Ramadhan Kessy kuitumikia timu yake hiyo lakini limeitaka Yanga kuzungumza na Simba.
Kessy alishindwa kuitumikia timu yake hiyo mpya aliyojiunga nayo mwanzoni mwa mwezi uliopita, lakini imeshindwa kumtumia katika mechi zake za makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga imecheza mechi nne na Jumamosi itacheza mchezo wa watano na Mo Bejaia ya Algeria huku ikiendelea kumkosa Kessy, Yanga ilionyesha jeuri na ilikataa kukaa mezani na Simba hivyo imepelea klabu ya Simba kudai mchezaji huyo hatocheza msimu mzima mpaka Yanga iwalipe shilingi milioni 62