Na Saida Salum, Dar es Salaam
Simba SC jana iliibamiza bila huruma AFC Leopards ya Kenya katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mabao 4-0 mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kuadhimisha Simba Day.
Magoli ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajibu (Mawili), Shiza Kichuya na Laudit Mavugo, mashabiki wa Simba wakaanza kuchonga na kuwaambia wenzao wa Yanga kazi wanayo na wakikutana nao Oktoba 1 mwaka huu watawapiga 5-0.
Lakini mashabiki wa Yanga bao wakawajibu wa Simba na kuwaambia wamecheza na timu dhaifu ambayo inakamata nafasi ya sita kutoka mkiani, kwa maana hiyo Leopards iko katika janga la kushuka daraja.
Simba kama ingecheza na Gor Mahia au Interclube ya Angola huenda wasingeshangilia kama wanavyoshangilia sasa, walisema mashabiki wa Yanga waliokuwa uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo