Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Mashabiki wa Simba wanatembea vifua mbele hasa baada ya timu yao jana kuichapa bila huruma AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, mchezo wa kuadhimisha tamasha la Simba Day.
Katika mchezo huo wa kirafiki Simba ilipata mabao yake kupitia kwa Ibrahim Ajibu 'Kadabla' aliyefunga mawili, Shiza Kichuya na Laudit Mavugo waliofunga moja moja, mara baada ya kumalizika mchezo huo tambo zilianza kutolewa na mashabiki wa Simba.
Wasikie watani zao Yanga wanachosema tena wakiwa na ushahidi mkononi, Kumbe Simba SC Ilicheza na timu dhaifu ambayo ilishindwa hata kulifikia lango la Simba, AFC Leopards inashikilia nafasi ya sita kutoka mkiani, kwa maana hiyo wanaweza kutelemka daraja