Hatimaye Simba na MO kimeeleweka

Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam

Kikao cha kamati ya utendaji cha klabu ya Simba kilichoketi Jumatatu kilichomkutanisha na mfanyabiashara mashuhuri barani Afrika Mohamed Gulam Dewji 'MO Dewji' kimeeleweka na sasa mambo yote shwari.

Taarifa za ndani kutoka kwenye kikao hicho ambapo Mambo Uwanjani imepata data, kwamba Kamati ya utendaji imeridhia kumkabidhi timu MO kwa sasa lakini ni kwa ajili ya kuisaidia tu huku mchakato rasmi wa kumuuzia ukiandaliwa.

Taarifa hizo zinasema kwa sasa MO Dewji ruksa kutoa chochote ndani ya Simba na anaweza kusafiri nayo ama kugharamia safari za Simba, Wakati mambo yakiwa shwari ndani ya Simba, Yanga wanazozana na bosi wao Yusuph Manji