Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) inamshikilia rais wa klabu ya Simba, Evans Elieza Aveva na amesekwa rumande katika kituo cha polisi Urafiki na muda wowote anaweza kufikishwa mahakamani.
Takukuru haijaweka wazi kama imemkamata Aveva kwa kosa lipi, lakini Mambo Uwanjani inafahamu kwamba Aveva amekamatwa na Takukuru kwa kosa la kuhamisha fedha za usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi katika akaunti yake binafsi.
Fedha za Okwi kutoka Etoile de Sportive Sahel ya Tunisia zilitumwa kwenye akaunti ya Simba lakini rais huyo alihamishia kwenye akaunti yake binafsi, kukamatwa kwa bosi huyo ni siku chache mara baada ya kukutana na mfanyabiashara Mohamed Gulam Dewji 'Mo' ambaye anataka kuinunua klabu hiyo, Mo alitoa shilingi milioni 100 za kusaidia usajiki