Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Azam yatangaza kikosi chake kamili, Farid nje, anakwenda Hispania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

USAJILI KAMILI AZAM FC

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha kubwa kuwatangazia kuwa imemaliza kikamilifu hatua ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao.

Katika hatua hiyo ya kwanza iliyofungwa Jumamosi iliyopita saa 6.00 usiku, Azam FC tumewasajili jumla ya wachezaji 21 na kuwatoa wengine sita kwa mkopo.

Wachezaji wapya walioingia katika orodha hiyo ni mabeki Bruce Kangwa anayetokea Highlanders ya Zimbabwe, Daniel Amoah kutoka Medeama ya Ghana pamoja na winga Enock Atta Agyei (Medeama).

Mbali na nyota hao watatu wa kigeni, wachezaji wa msimu uliopita waliofanikiwa kupenya kwenye orodha hiyo ni makipa Aishi Manula, Mwadini Ally, mabeki Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Pascal Wawa, David Mwantika na kinda Ismail Gambo ‘Kusi’.

Viungo ni Nahodha Msaidizi, Himid Mao ‘Ninja’, Jean Mugiraneza ‘Migi’, Michael Bolou, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya, Frank Domayo ‘Chumvi’, mawinga Ramadhan Singano ‘Messi’, Khamis Mcha ‘Vialli’ na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’, ambaye ndiye Nahodha Mkuu wa kikosi.

Wanaotoka kwa mkopo 

Azam FC inayodhaminiwa na Benki na NMB na kinywaji safi kabisa cha Azam Cola, katika kukuza vipaji vya wachezaji wetu, tumeamua kuwatoa kwa mkopo nyota wetu wengine sita kwenda timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na barani Ulaya.

Waliotolewa kwa mkopo hapa nchini, ni beki Abdallah Kheri tuliyempeleka Ndanda FC pamoja na kiungo Bryson Raphael, ambaye aliichezea timu hiyo msimu uliopita katika mzunguko wa pili na kuifungia mabao mawili.

Wengine ni winga Joseph Kimwaga aliyekwenda Mwadui baada ya kutakiwa na Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, pamoja na washambuliaji Kelvin Friday aliyerejea Mtibwa Sugar na Ame Ally ‘Zungu’, aliyekwenda Simba.

Farid kutua Tenerife

Habari njema zaidi, tayari wamefikia makubaliano na Klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania (sawa na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara), juu ya winga wa kushoto Farid Mussa, waliyekuwa wakimuhitaji baada ya kufuzu majaribio ya kujiunga nao miezi mitatu iliyopita.

Hivyo, Farid hatakuwa sehemu ya kikosi chao msimu ujao na anakwenda Tenerife ya huko, ambapo Azam FC kwa kutambua kipaji cha kijana wetu tumeamua tumwachie akajiunge na kikosi hicho kwa makubaliano maalumu na hatujachukua fedha yoyote kwa sasa lengo ni kuona kipaji chake kikikua zaidi na tunapenda kumtakia mafanikio mema huko anapokwenda.

'Tunaamini mafanikio yake yoyote huko, atakuwa amelitangaza vema jina la Azam FC na kadiri atakavyokuwa akizidi kusonga mbele basi hapo ndipo klabu yetu itakuwa ikinufaika zaidi kupitia biashara hiyo', ilisema taarifa hiyo.

Usajili hatua ya pili

Katika kumalizia taratibu zote za usajili kwa msimu ujao, Azam FC bado wanaendelea na zoezi hilo la usajili kwa hatua ya pili likihusisha wachezaji wa kigeni, ambalo litaanza rasmi Agosti 17 hadi Septemba 7, mwaka huu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC