Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Mshambuliaji Atupele Green aliisawazishia timu yake ya JKT Ruvu, ikiwabana mbavu nyumbani Azam FC ya kufungana mabao 1-1 mchezo wa kirafiki.
Atupele ambaye alikuwa akiwaniwa pia na Simba SC, aliisawazishia timu yake katika kipindi cha pili, Azam walikuwa wa kwanza kujipatia bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza likifungwa na beki wake Agrey Morris kwa mkwaju wa penalti.
Katika mchezo huo beki Shomari Kapombe alicheza kwa mara yake ya kwanza tangu baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika Kusini