Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
AZAM FC kwa mara ya kwanza leo imetwaa Ngao ya Jamii baada ya kuitandika Yanga SC mabao 4-1 kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Yanga watabidi wajilaumu wenyewr hasa baada ya kuongoza kwa mabao mawili hadi mapumziko, magoli ya Yanga yote mawili yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wake raia wa Zimbabwe Donald Dombo Ngoma huku moja akifunga kwa mkwaju wa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa.
Kipindi cha pili Azam walifanya mabadiliko mazuri na kufanikiwa kukomboa mabao yote mawili, Shomari Kapombe alianza kuifungia Azam bao la kwanza, kabla ya nahodha John Bocco "Adebayor" kusawazisha kwa mkwaju wa penalti.
-
Hadi mwisho matokeo ni sare ya 2-2 ndipo timu hizo zilipokwenda kwenye mikwaju ya penalti ambapo Azam ikawa mabingwa kwa kufunga penalti nne na Yanga wakapata moja huku wakipoteza mbili zilizopigwa na Hassan Kessy na Haruna Niyonzima, Hii ni ndoo ya kwanza kwa Azam na inaashiria msimu huu mpya utakuwa mzuri kwao