Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kupambana na rushwa nchini (Takukuru) imesema, rais w klabu ya Simba, Evans Aveva alihusika kuhamishia fedha za klabu zipatazo milioni 600 katika akaunti yake binafsi kutoka akaunti ya klabu.
Pia rais huyo alituma Hong Kong China Dola 62'000 ambapo sasa Takukuru inawasiliana na wenzao wa Hong Kong ili kujua fedha hizo zimetumikaje.
Aveva alishikiliwa katika kituo cha polisi cha Mabatini, Kijitonyama kwa siku mbili akidaiwa kukwapua fedha za usajilj wa mshambuliaji Emmanuel Okwi, fedha hizo zilitumwa na Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo ilikuwa ikidaiwa baada ya kumsajili bila kuilipa Simba mpaka pale iliposhitaki FIFA ambayo nayo iliiagiza Etoile kuilipa Simba ama sivyo watawashusha daraja