Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) imemwachia kwa dhamana rais wa klabu ya soka ya Simba, Evans Elieza Aveva baada ya kumshikilia kwa muda wa siku mbili.
Aveva alikamatwa juzi na maafisa wa Takukuru na alifikishwa katika kituo cha polisi cha Urafiki kilichopo Ubungo, bosi huyo wa Simba alihojiwa na taasisi hiyo kwa makosa ya kuhamisha fedha za klabu yake kwenye akaunti yake binafsi.
Kamati ya utendaji na viongozi wengine wa klabu hiyo nao walihojiwa na Takukuru na baada ya kujiridhisha ikawaachia na rais Aveva naye akapewa dhamana awali Takukuru ilikataa kumwachia kwa dhamana mpaka pale itakapokamilisha uchunguzi