Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa timu ya Vital' 0 ya Burundi pamoja na timu ya taifa ya nchi hiyo Laudit Mavugo amewatumia salamu wapenzi na mashabiki wa Simba SC kwamba anakuja hivi karibuni kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.
Akizungumza leo kutokea Bujumbura, Mavugo amesema anatarajia kujiunga na Simba na mazungumzo yake na uongozi wa Simba yanakwenda vizuri.
"Ni kweli nakuja Simba na nitasaini mkataba wa miaka miwili, Wapenzi na mashabiki wa Simba watulie tu mimi ni wao msimu ujao", amesema mshambuliaji huyo ambaye ni mfungaji bora wa ligi ya Burundi.
Simba wamekuwa wakimuhitaji kwa muda mrefu mshambuliaji huyo hivyo kwa kauli yake hiyo itapelekea furaha kwa wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo iliyopepesuka kwa misimu minne mfululizo ikikosa ubingwa