SAMATTA ATUPIA BAO LAKE LA KWANZA UBELGIJI

Na Mwandishi Wetu

Mtanzania Mbwana Samatta leo amefungua akaunti yake ya mabao baada ya kuifungia bao la ushindi timu yake mpya ya KRC Genk inayoshiriki ligi kuu Ubelgiji.

Mbwana Samatta aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, alifunga bao hilo kunako dakika ya 81 zikiwa ni dakika mbili tu tangia aingie akitokea benchi.

Samatta ameiwezesha timu yake hiyo kushinda 3-2 na kuondoka na pointi tatu muhimu katika ligi kuu ya Ubelgiji

Hilo ndiyo goli lake la kwanza tangu alipojiunga na timu hiyo, Samatta alikuwa mfungaji bora na pia mchezaji bora wa Afrika, tuzo aliyoshinda mwishoni mwa mwaka jana