Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amegeuka mbogo na kushusha lawama za wazi kwa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Kilimanjaro Stars, chini ya Abdallah King Kibadeni, kwa kusema kuwa anaua viwango vya wachezaji wake. Mdachi huyo akiwa na sura ya hasira, alilalamikia kitendo cha kipa wake tegemeo, Ally Mustapha ‘Barthez’ kupigwa benchi mwanzo mwisho kwenye michuano ya Kombe la Chalenji huko Ethiopia, hadi Kili inatupwa nje ya michuano hiyo kwa kile alichodai ni makosa aliyoyafanya kwenye mchezo na Algeria. Barthez alilazimika kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria, baada ya kuonekana kuwa uchochoro siku hiyo ambayo Stars ililala mabao 7-0. Akifafanua kauli yake, Pluijm alisema siku zote kocha ni sawa na mzazi, hivyo kumpotezea namna hiyo ni kummaliza kabisa kwani mwishowe atashindwa kujiamini.
Kwa habari na matangazo tunapatikana Kariakoo jijini Dar es Salaam au piga +255 652 626627 au +255 755 522 216 barua pepe princehoza@gmail.com