Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ZIARA YA PAPA AFRIKA MASHARIKI: Papa Francis: Dini isitumiwe kuvuruga amani



Papa Francis ameongoza ibada ya misa ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo amesisitiza umuhimu wa familia katika jamii.

Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga akisema “Mungu ni Mungu wa amani.”

"Jina lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika.

Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la dini kupanda woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.

"Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguse nyoyo za wanaohusika katika mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu."


Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa makanisa mengine akiwemo kiongozi wa Kanisa la Kiangilikana Kenya Dkt Eliud Wabukala.

Viongozi wa dini ya Kiislamu Kenya pia wamehudhuria mkutano huo, wakiongozwa na Prof Abdulghaful El-Busaidy.

Papa Francis amesema amekuwa akihakikisha kila aendako anatangamana na watu wa dini na imani nyingine.
Image caption Baada ya misa, waumini waliendelea kupokea komunyo

"Huwa ni muhimu sana kwangu kwamba, ninapofika pahali kutembelea waumini wa kanisa Katoliki, ninakutana na viongozi wa makanisa mengine na dini nyingine. Natumai kuwa wakati ambao tumekuwa pamoja utakuwa ishara ya matamanio ya Kanisa kwa dini zote, ninaomba ikaweza kuimarisha urafiki ambao tayari tunajivunia,” amesema.

Wakati wa ibada ya misa ambayo ilianza saa nne asubuhi, Papa Francis alisisitiza umuhimu wa familia katika jamii na kupinga utoaji wa mimba.

“Afya ya jamii yoyote hutegemea afya ya familia. Kwa ajili yake, na kwa ajili ya jamii, Imani yetu katika neno la Mungu inatuita tuunge mkono familia katika jamii, kuwakubali watoto kama Baraka kwa ulimwengu, na kutetea hadhi ya kila mtu, kwa ndugu zetu wote katika familia moja ya binadamu,” amesema.
Image caption Baadhi ya waumini walitoka Afrika Kusini

“Kwa kutii neno la Mungu, tunahimizwa kuachana na matendo ambayo yanachochea udhalimu miongoni mwa wanaume, kuumiza au kudumisha wanawake, na kutishia maisha ya watoto ambao hawajazaliwa ambao hawana hatia.”

Watu waliohudhuria ibada hiyo walianza kuingia uwanjani mapema na walivumilia mvua ambayo ilianza kunyesha mapema asubuhi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...