Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KERR MBISHI NA HASHAURIKI- MATOLA

Ilianza kama utani, lakini hatimaye juzi usiku  ikawa kweli baada ya Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba, Selemani Matola kutangaza rasmi kutema kibarua hicho.

Matola, beki wa zamani wa klabu hiyo, amesema amefikia uamuzi huo baada ya kushindwa kuelewana na bosi wake, Kocha Mkuu, Dylan Kerr.

Akizungumza muda mfupi baada ya kujiondoa Simba usiku wa kuamkia jana, Matola alisema tabia ya ubishi na kutoshaurika kwa Kocha  Kerr ndiyo sababu iliyom kimbiza Msimbazi.

Alisema uongozi wa Simba una taarifa za kuondoka kwake, kwani alifanya hivyo baada ya kikao kilichoongozwa na Rais wa Simba, Evans Aveva juzi usiku.

“Nimeamua kukaa pembeni, mambo yalikuwa yanazidi kuwa magumu, nilikutana na Evans tangu saa mbili usiku (juzi usiku), tumeongea lakini, msimamo wangu ulikuwa palepale,” alisema Matola,  kiungo  wa zamani wa RTC Kagera na Super Sport ya Afrika Kusini.

Aliongeza: “Msimamo wangu ni kujiondoa kabisa kufundisha Simba kwa sasa, sitaki hata kwenda timu B.”

Alisema mara kadhaa amekuwa akiripoti kwa uongozi kwa klabu kuhusu kutofautiana kwake na Kerr, lakini jambo la kushangaza hakuna suluhisho lolote lililofikiwa.


“Ratiba yake ya mazoezi hairidhishi kabisa, nilimweleza rais (Aveva) na alikuja kwa siri kwenye mazoezi na kushuhudia ukweli, lakini hakuna alilofanya hadi sasa,” alisema.

Alisema ni jambo la kushangaza kwa klabu kubwa kama Simba kufanya mazoezi mara moja kwa siku wakati inakabiliwa na mechi ngumu ligi kuu.

 “Timu inapaswa kufanya mazoezi mara mbili kwa siku--asubuhi na jioni, lakini Kerr kwake siyo hivyo. Mazoezi ni asubuhi tu, ukimshauri kinyume inakuwa tabu,” alisema.

Kuhusu kiwango cha timu hiyo, alisema ni udhaifu kutokana na ukweli kwamba wachezaji wanapumzika muda mwingi badala ya kufanya mazoezi.

“Mazoezi ni muhimu sana kwa mchezaji na kadri anavyofanya mazoezi mara kwa mara ndivyo anavyojenga stamini na uwezo.

“Tulipokuwa Mbeya, nilishindwa kumvumilia alipobadili wachezaji saba katika kikosi kilichoshinda dhidi ya Mbeya City, akapanga timu yake na matokeo tulifungwa. Tuliporudi Dar niliueleza uongozi, lakini ukawa kimya hadi napotangaza kujiondoa,” alisema Matola.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Haji Manara alisema uongozi utakutana katika kikao cha dharura kujadili hali ilivyo ndani ya klabu.

Matola alikuwa kocha wa vijana wa klabu hiyo tangu 2010 na baadaye kupandishwa cheo na kuwa Kocha Msaidizi kwa makocha Patrick Phiri (Zambia), Zdravko Logarusic (Croatia) na Goran Kopunovic (Serbia).

BAADA YA KUJIONDOA

Matola alisema kwa sasa yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Bulyanhulu ya Shinyanga na wakiafikiana ataanza kuinoa timu hiyo inayocheza Ligi Daraja la Kwanza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC