Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KERR ATAMBA KUENDELEZA UBABE MBEYA


Baada ya kuvunja mwiko wa kuwa kibonde wa Mbeya City katika misimu miwili iliyopita, benchi la ufundi la Simba limetamba litaendeleza kaulimbiu ya 'mabadiliko' inayotamba nchini kwa sasa kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya keshokutwa.

Simba ililazimishwa sare na Mbeya City katika mechi zote mbili za msimu wa kwanza (2013/14) wa timu hiyo ya Mbeya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), kabla ya kuchezea kichapo katika mechi zote mbili za msimu uliopita wa ligi hiyo, 2-1 nyumbani na 2-0 ugenini, lakini juzi Wanamsimbazi walianza na kikosi chenye viungo watano, Said Ndemla, Jonas Mkude, Abdi Banda, Mwinyi Kazimoto na  Justice Majabvi na kuchomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya
timu hiyo mjini hapa.

Kwa safu hii, Simba inaweza kabisa kuondoka na pointi zote sita mbele ya Prisons

Ushindi huo ni mwendelezo wa mabingwa hao mara 18 wa Bara kufanya mabadiliko baada ya mwanzoni mwa msimu kuvunja mwiko wa kugawa pointi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kwa misimu mitatu, safari hii wakichukua pointi sita kutoka kwa African Sports na Mgambo Shooting.

Mara tu baada ya kumalizika kwa mechi yao ya juzi jijini hapa, kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola, aliiambia Nipashe kuwa Tanzania Prisons ambao ambayo juzi ilisambaratishwa kwa kipigo kikubwa cha mabao 3-0 dhidi ya Stand United mjini Shinyanga, ijiandae kukumbwa na mabadiliko ya Msimbazi keshokutwa.

"Tumecheza vizuri kipindi cha kwanza, kipindi cha pili hali ya hewa ilitusumbua, lakini muhimu ni pointi tatu kwa sababu uwanja huu (Sokoine) umekuwa mgumu kwetu kwa kipindi kirefu. Tuko hapa Mbeya kwa ajili ya kuvunja mwiko na kupata pointi sita. Tayari tumepata tatu kwa Mbeya City, tunazisubiri pointi tatu nyingine kutoka kwa Prisons Jumatano," alitamba Matola.

Kuhusu mchezaji wa zamani wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' ambaye juzi alicheza kwa mara ya kwanza VPL akiwa na kikosi cha City, Matola alisema: Hakuna asiyejua Boban ni mchezaji mzuri, tatizo linalomsumbua kwa sasa ni kwamba amenenepa, lakini akifanya mazoezi, atawasaidia sana Mbeya City."

Katika hatua nyingine, kocha mkuu wa Simba, Dylan Kerr, amekiponda kikosi chake kwa kuonyesha kiwango duni kwenye mechi yao ya juzi dhidi ya City.

Katika mahojiano jijini hapa jana, Muingereza huyo alisema: "Sijafurahishwa na namna timu ilivyocheza dhidi ya Mbeya City. Tulizidiwa kwa kiasi kikubwa, goli na ushindi pekee ndicho kitu cha kufurahia hapa, hatukucheza hivi kwenye mazoezi. Mechi haikuwa na furaha kwangu kwa sababu tumecheza soka la Amerika."

Kocha wa Mbeya City, Abdul Mingange, aliliambia gazeti hili jijini hapa juzi kuwa ili timu yake ifanye vizuri VPL msimu huu, watalazimika kusaka washambuliaji wakali wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi ujao.

"Tumetengeneza nafasi nyingi za mabao, lakini safu yetu ya ushambuliaji imetuangusha. Tunatakiwa kulitumia vyema dirisha dogo kuongeza washambuliaji," alisema meja huyo mstaafu ambaye msimu uliopita alikinoa kikosi cha Ndanda FC ya Masasi, Mtwara.

MECHI ZIJAZO..  
    
Oktoba 21, 2015
Yanga SC Vs Toto Africans
Stand United Vs Majimaji FC
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
Prisons Vs Simba SC
Coastal Union Vs Kagera Sugar
Oktoba 22, 2015
Ndanda FC Vs Azam FC
Mwadui FC Vs Mgambo Shooting
Mbeya City Vs African Sports

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC