Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NAHODHA SIMBA, ATAMBA KUTOIOGOPA YANGA

NAHODHA wa Simba SC, Mussa Hassan Mgosi amesema kwamba akili zao zipo kwenye mechi yao ya Jumapili dhidi ya Kagera Sugar na hawaumizwi kichwa hata dogo na mahasimu wao, Yanga SC.

Akizungumza juzi mjini Tanga, Mgosi amesema baada ya kushinda mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara sasa wanaelekeza nguvu zao katika mchezo wa tatu dhidi ya Kagera.
“Sioni sababu ya kuwazungumzia Yanga kwa sasa wakati mechi ijayo tunacheza na Kagera. Kwanza nataka nikuambie, hao Yanga hawatuumizi kichwa kabisa,”amesema.

Mgosi amesema kwamba wachezaji wote wa Simba SC kwa sasa akili yao inafikiria namna gani wataifunga Kagera Sugar ili kufikisha pointi tisa ndani ya mechi tatu.

Simba SC imeanza vyema Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushinda mechi zake zote mbili za mwanzo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga 1-0 dhidi ya African Sports na 2-0 dhidi ya JKT Mgambo.


Sasa Wekundi hao wa Msimbazi walio chini ya kocha Muingereza, Dylan Kerr watacheza mechi yao kwanza nyumbani mwishoni mwa wiki, dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


MECHI ZIJAZO LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA

Septemba 19, 2015
Stand United Vs African Sports
Mgambo Shooting Vs Majimaji FC
Prisons Vs Mbeya City
Yanga SC Vs JKT Ruvu
Septemba 20, 2015
Mwadui FC Vs Azam FC
Mtibwa Sugar Vs Ndanda FC
Simba SC Vs Kagera Sugar
Coastal Union Vs Toto Africans
Septemba 26, 2015
Simba SC Vs Yanga SC
Coastal Union Vs Mwadui FC
Prisons Vs Mgambo Shooting
JKT Ruvu Vs Stand United
Mtibwa Sugar Vs Majimaji FC
Kagera Sugar Vs Toto Africans
Septemba 27, 2015

African Sports Vs Ndanda FC
Azam FC Vs Mbeya City

Chanzo Bin Zubeiry

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC