Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAKALA: Halifa Maliyaga: Msanii anayekuja juu bongo muvi


Na Prince Hoza

ONGEZEKO la vijana katika tasnia ya sanaa hasa filamu limezidi  kukua kwa kasi, hii inadhihirisha kuwa vijana wengi hawana  ajira na sasa filamu zinaweza kuwaokoa.

Halifa Yuda Maliyaga ( Pichani) ndiyo jina lake halisi, naye ameamua  kujikita kwenye tasnia hiyo lakini yeye anadai sanaa hiyo ipo  ndani ya damu ya ukoo wao kwani kaka yake Hemed Halifa  Maliyaga maarufu 'Mkwere' anatesa kwenye kundi la Mizengwe.

Maliyaga aliingia rasmi kwenye sanaa baada ya kumaliza shule  ya msingi mwaka 2011 katika shule ya Mdaula Chalinze Pwani,  kundi lake la kwanza kushiriki nalo linaitwa Zinduko Arts  ambapo alidumu nalo hadi mwaka 2014.

Maliyaga alijiunga na kundi la Nuru njema Arts Group mwaka  2014 ambapo anatamba nalo hadi sasa.


NINI KILIMSUKUMA KUINGIA KWENYE SANAA HIYO


Moja ya sababu zilizomfanya aipende tasnia hiyo ni ushawishi  mkubwa baada ya kumuona ndugu yake Hemed Halifa maarudu  'Mkwere' akitamba katika fani hiyo/

Amesema katika kipindi hiki toka awepo kwenye sanaa ya  uigizaji ameshashiriki kurekodi filamu nne ambazo alizitaja ni  'Tandu', 'Mti wa ajabu', 'Bonge la utata' na 'Mfalme puto'  ambao unatarajia kutoka baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu  Ramadhani.

CHANGAMOTO

Maliyaga amesema changamoto ni nyingi kwa wasanii chipukizi  kama wao lakini kikubwa ni nidhamu na uvumilivu, na amemtaja  msanii Gabo kwamba ndiye anayemvutia.

Amemaliza kwa kusema, lengo lake ni kuwa mmoja wa wasanii  wakubwa katika nchi hii kama ilivyo kwa kaka yake Mkwere  anayetesa ITV na kundi lake la Mizengwe.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC