Ruka hadi kwenye maudhui makuu

WAJERUMANI WASIKITISHWA NA BALLON D'OR

Manuel Neuer

Wajerumani, waliotumai wangefagia tuzo za Fifa na kubeba Ballon D'Or, walieleza masikitiko yao Jumanne baada ya kipa wao aliyeshinda Kombe la Dunia Manuel Neuer kuibuka wa tatu katika matokeo ya mchezaji bora wa mwaka duniani wa mwaka 2014.

Mreno Cristiano Ronaldo alishinda tuzo hiyo kwa mara ya pili mtawalia Jumatatu na mara ya tatu kwa jumla.
Fowadi huyo wa Real Madrid alipata kura maradufu kumshinda mpinzani wake wa jadi aliyeshinda tuzo hiyo mara nne Lionel Messi, ambaye alimpiku pembamba kipa wa Bayern Munich Neuer aliyemaliza wa tatu.

Neuer, aliyewika sana katika Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana na pia alisaidia Bayern kushinda ligi na kombe nyumbani, amefungwa mabao manne pekee katika mechi 17 alizocheza ligini msimu huu.


“Nadhani si haki,” alisema nahodha na kocha wa zamani wa Ujerumani aliyeshinda Kombe la Dunia Franz Beckenbauer.
"Inaonekana kana kwamba katika kura hii ufanisi hauthaminiwi sana kama sura.”
"Makipa wamo katika pahala pagumu. Watu wanataka kuona mabao, si watu wanaozuia magoli yasifungwe.”

Ujerumani ilikuwa ikitarajia kufagia tuzo usiku huo baada ya kocha wa timu ya taifa Joachim Loew kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka naye kocha wa VfL Wolfsburg Ralf Kellermann akatawazwa kocha bora wa soka ya wanawake.

Kiungo wa Wolfsburg Mjerumani Nadine Kessler alichaguliwa mchezaji bora wa mwaka wa kike.
“Nimetamaushwa kiasi kumhusu Manuel," Loew aliambia wanahabari. “Kwa sababu katika Kombe la Dunia Manuel alionyesha mchezo tofauti sana wa kulinda wavu na ni jambo ambalo halijawahi kufanyika awali.”
Neuer alitawazwa kipa wa mwaka 2014 baada ya ustadi wake Kombe la Dunia, ambapo alitoka sana eneo la hatari na kufagia wapinzani tofauti na makipa wengine wa awali.

Lakini hakuungwa mkono hata na wachezaji wenzake wa Bayern, straika wa Poland Robert Lewandowski, kwa mfano akimpigia kura Mreno Ronaldo.

"Lilikuwa kosa kwangu kumpigia kura Ronaldo," Lewandowski aliambia wanahabari baadaye. “Leo ningempigia kura Manuel lakini kura yangu niliipiga Agosti. Ningepiga kura tofauti leo.”
Kwa Neuer, hata hivyo, ulikuwa usiku wa kufana hata bila yeye kushinda tuzo hiyo.

“Naondoka kutoka kwa jengo hili nikiwa na tabasamu kuu usoni. Ilikuwa siku ya ushindi kwangu na ulikuwa ufanisi kuwa kwenye tatu bora,” alisema. “2014 ulikuwa mwaka wa ufanisi mwingi na utasalia daima akilini mwangu.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC