Ruka hadi kwenye maudhui makuu

LIGI KUU BARA KIVUMBI NA JASHO LEO, SIMBA, YANGA AU AZAM KUCHEKA?

BAADA ya michuano ya Kombe la Mapinduzi, sasa kazi inarejea kwenye. Ligi Kuu Bara.Michuano ya wiki ya Kombe la Mapinduzi mjini Zanzibar tayari imepata mbabe wake, Simba na kombe liko jijini Dar es Salaam.

Vita ya vinara Mtibwa Sugar, Azam, Yanga na Simba ambao wote wana viporo katika michuano ya ligi kuu, kutokana na kuwepo katika ushiriki wa michuano ya Mapinduzi, lakini wikiendi hii- leo na kesho wanaendelea kumsaka mwali wa Ligi Kuu Bara ambaye anahifadhiwa na Azam FC.

Kila upande una hofu, inajulikana kwa kuwa matokeo hayana uhakika. Mechi za mwisho zinaonyesha Yanga na Azam waliambulia sare, hali kadhalika Mtibwa Sugar wakati Simba walikutana na kichapo.


Yanga Vs Ruvu Shooting

Hata hivyo kwa jicho la harakaharaka, mechi za wikiendi hii zimejawa hofu kwa timu zote zinazokutana, huku kubwa ikiwa ni ya Yanga dhidi ya ‘vibonde’ wao wa msimu uliopita, Ruvu Shooting ambayo ilinyweshwa mabao 7-0, ukiwa ni ushindi wa rekodi ya msimu. Pia vinara wanaokabana kileleni, Mtibwa Sugar na JKT Ruvu, inatafsiriwa ni nguo kuchanika kutokana na kila moja kutaka kubaki kileleni mwa msimamo.

Azam vs Stand United (Kambarage)

Mabingwa watetezi, Azam wanaingia uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya kutofanya vema kwenye michuano ya Kombe la Mapunduzi na kutupwa nje hatua ya robo fainali na Mtibwa Sugar.

Hata hivyo wikiendi hii ni kipindi cha kocah Joseph Omog kurejesha imani kwa viongozi wake kwani Azam ni moja ya timu zenye kila aina ya staa tena wa bei ghali lakini matokeo yake haijafanya vema kulinganisha na thamani yao.

Ni mechi ya kufia uwanjani, kwani Stand ambao ni wanaingia na hasira za kupoteza mchezo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi walipochapwa na JKT Ruvu, wikiendi iliopita.

Yanga vs Ruvu Shooting (Taifa)


Moja ya mechi yenye hisia nyingi pande zote. Wakati Yanga wakiingia kwa kujihami kwa ushindi wa rekodi ya msimu wa mabao 7-0 waliovuna msimu uliopita, wanajeshi wa Ruvu Shooting wao wanasema ni kipindi cha kulipiza kisasi hata kama si cha idadi ya mabao hayo.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga imezidi kuwa moto wa kuotea mbali hasa wakifanya maajabu kwenye Mapinduzi, ambapo waliweka rekodi ya kufunga mabao tisa katika mechi tatu.

Hata hivyo Ruvu wao wanasema ujio wa George Michael ‘Kifaru’ ambaye alikuwa ‘homa’ ya mastraika ni chachu ya kuwapunguza kasi akina Simon Msuva. Pia Ruvu wana hasira za kuchapwa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mgambo Shooting, matokeo yaliyowaweka nafasi ya tisa, hivyo kufungwa leo tena ina maana watakuwa na hali ngumu zaidi.

Ndanda vs Simba (Nangwanda Sijaona)

Itapigwa leo pia huko Kusini mwa nchi, lakini si mechi yelele mama pande zote. Simba wanaingia wakiwa na furaha ya ubingwa wa Mapinduzi, lakini pia hapohapo wakilizwa na matokeo mabovu kwenye ligi kuu.

Simba haihitaji kubeza mchezo huu kwa kujidanganya na taji lao, badala yake akili yote ihamie kwenye matunda walio nayo ligi kuu. Hata hivyo Ndanda wamekuwa wagumu zaidi kwa timu vigogo kwenye Uwanja huo, ambapo mabingwa watetezi Azam walikubali kichapo cha bao 1-0 msimu huu.

Hivyo watauingia kwa tahadhari ya juu kuhusu ugumu wa uwanja huo vinginevyo wanarudi mjini vichwa chini.

Kagera vs Mbeya City (CCM Kirumba)


Nalo ni ‘goma’ la wiki hii. Timu zote zitakuwa ugenini, unaweza kusema ni uwanja ‘neutral’ kutokana na uwanja wa nyumbani wa Kagera Sugar, Kaitaba kuwa kwenye matengenezo hivyo mchezo kuhamishiwa mkoa jirani wa CCM Kirumba, Mwanza.

Timu zote ‘zime-relax’ sana kutokana na kutokuwa na mechi kufuatia ratiba ya Mapinduzi. Zina rekodi sawa kwani msimu uliopita zilitoshana nguvu mechi zote mbili.

Lakini Mbeya City wanajua Kagera Sugar wako ‘on fire’ baada ya kutoka kuitwanga Simba kwa bao 1-0 katika mechi ya ugenini. Hivyo bado Kirumba haiwezi kuwa ugenini sana kwao na vijana wa Juma Mwambusi wanatakiwa kuwa makini kweli.

Mgambo Vs Prisons

Uwanja wa Mkwakwani hautapumzika kwa siku mbili mfululizo wakati Mgambo ikiwa mwenyeji wa Prisons katika mechi itayotarajiwa kuwa ngumu na yenye kutumia nguvu nyingi sana kwa kuwa kila upande wako fiti kweli.

Kesho, kutakuwa na kazi nyingine wakati Wagosi wa kaya Coastal Union wakiwakaribisha Polisi Moro, moja ya timu inayocheza soka safi na la kitabuni.

Coastal licha ya kutokuwa katika tatu bora katika msimamo ni moja ya timu yenye kikosi chenye wachezaji wazuri wa kigeni kutoka katika nchi za Nigeria, Uganda na Kenya.

Lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kuisimamisha Polisi kabla ya dakika 90 ambazo ndiyo zitatoa jibu na lazima kazi ifanyike.

JKT Ruvu Vs Mtibwa (Chamazi Complex)

Pia kesho kutakuwa na mechi nyingine ‘ngangari’ wakati vinara wa ligi hiyo, Mtibwa Sugar watakapokuwa wakitafuta pointi zaidi safari hii wakiwa ugenini dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi itapigwa kwenye Uwanja wa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam. Itakuwa moja ya mechi ngumu na Mtibwa wanapaswa kuwa macho kweli maana wanajeshi hao sasa hawatabiriki.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC