Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAKALA: YAJUE MAISHA YA JONAS MKUDE WA SIMBA SC

TANZANIA ina jumla ya watu milioni 45 kulingana na sensa ya watu ya mwaka 2012, kati yao kuna wanandinga lukuki, lakini ina kiungo mmoja tu mkabaji anayeaminiwa na wengi ambaye si mwingine ni Jonas Gerald Mkude utotoni alikuwa akiitwa Jonas Mwakindagi.

Wengi hawaijui historia ya Mkude lakini gazeti la Msimbazi limefanikisha kuipata na hatimaye leo inawajuza, alipokuwa mdogo akicheza mpira wa chandimu, Mkude alianzia golini.

Timu ya mtaani kwake iliyoanzia kucheza barabarani na kupelekea usumbufu mkubwa kwa wapita njia, hasa watembea kwa miguu, baiskeli au magari na pikipiki, Mkude na akiwa na umri wa miaka minne alisimama imara katika lango la timu yake.

Kipindi hicho alipata usumbufu mkubwa kutoka kwa mama yake ambaye hakutaka mwanaye acheze soka, lakini alijiiba mara kwa mara na kuendelea nao.


Mkude alikuwa akipenda sana soka kuliko michezo mingine na inasemekana alionyesha mapenzi na timu yake ya Simba tangia akiwa mdogo, alianza rasmi kuupneda mchezo huo akiwana miaka minne.

Mama mzazi wa kiungo huyo Grace Ambrosse Shimba alimwelezea mwanaye kuwa alijitahidi kumzuia asicheze soka lakini ikashindikana, 'Kikubwa nilikuwa nahofia mwanangu asiumie kwani maisha yangu yalikuwa magumu sana isitoshe nimemlea mwenyewe', alisema mama huyo ambaye anaishi Kinondoni B mtaa wa Kisutu.

Jonas Mkude alizaliwa mwaka 1992 Kinondoni B na makuzi yake yalikuwa huko huko Kinondoni, alianza elimu ya msingi mwaka 1998 katika shule ya Hananasif na kumaliza mwaka 2005.

Aliendelea na masomo ya sekondari mwaka 2006 katika shule ya Kambangwa hadi mwaka 2009 alipomaliza, kama nilivyoanza kukuelezea hapo awali Mkude alijikita rasmi kwenye soka la ushindani, ambapo kipaji chake kiligundulika akiwana umri wa miaka minne.

Mjomba wa mwanandinga huyo anamuelezea Mkude kuwa alipogundua kipaji cha mpwawe alikuwa akimuamsha alfajili ili awahi mazoezini na alipokuwa shuleni hasa kidato cha kwanza pale Kambangwa sekondari kipaji chake kilizidi kuongezeka.

Mjomba wa mchezaji huyo anamtaja Mkude kuwa amelelewa kwa babu na bibi ambao wote ni marehemu hivyo wakati wote walikuwa naye na kila aliporudi nyumbani kutoka shule husimulia matokeo yake ya darasani pamoja na uwanjani pia.

Mkude alianza kuzivutia timu mbalimbali zilizokuwa zikimfuatilia, lakini akaeleza kuwa muda wote alijulikana kwa jina la Jonas Mwakindagi na siyo Jonas Mkude kama ilivyo sasa.

Timu ya kwanza kabisa kubisha hodi na kumchukua Mkude ilikuwa Mwanza United ya Mwanza ambapo alijiunga na timu hiyo iliyokuwa ikishiriki ligi dadaja la kwanza Tanzania bara, kwakuwa timu hiyo ilikuwa ikimchenga kummalizia fedha zake za usajili aliachana nayo, Mkude alidumu na timu hiyo kwa mwaka mmoja tu.

SAFARI YA KUELEKEA SIMBA SC YAIVA 

Jonas Mkude akiwajibika uwanjani

Baada ya kuachana na Mwanza United ya Mwanza, Mkude alijiunga na timu ya Kombaini ya Hananasif ya Kinondoni, timu hiyo ilifanya ziara yake ya kimichezo jijini Arusha ambapo ilikwenda kwa mwaliko maalum.

Ikiwa Arusha, viongozi wa Simba SC ilituma wajumbe wake ili kumfuatilia kijana huyo, kumbe Simba ilianza kumvizia Mkude tangia anasoma darasa la sita katika shule ya Hananasif.

Simba SC ilimsaini Mkude na kuamua kumpeleka katika kikosi chake cha pil Simba B, kwakuwa umri wake ulikuwa mdogo walimuahidi watampandisha kikosi cha wakubwa hapo baadaye.

Akiwa Simba B, Mkude aliiwezesha kutwaa kombe la Uhai linaloshirikisha vikosi vya pili vya timu zinazoshirki ligi kuu bara, Mkude ambaye alionyesha uwezo mkubwa katika michuano hiyo alikuwa miongoni mwa wachezaji watano waliopandishwa katika kikosi cha wakubwa.

Makocha wote walioinoa timu hiyo hakuna hata mmoja ambaye aliyeshindwa kumuanzisha katika kikosi cha kwanza, Mkude pia ni mchezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars na amekuwa mhimili mkubwa kwenye timu hiyo.

Akiwa amepozi nje  ya bustani wakati apolikuwa majeruhi

Siku za hivi karibuni, nyota yake imezidi kung'ara na kupelekea kugombewa na karibu timu tatu ikiwemo Simba SC, timu nyingine zilizokuwa zikimtaka ni Yanga SC na Azam FC, timu hizo ziliingia vitani kumuwania baada ya mkataba wake na Simba kumalizika.

Simba SC ilifanikiwa tena kumpata na kumuongezea mkataba wa miaka miwili, huku akipewa gari la kifahari na pesa taslimu zaidi ya milioni 70 za Kitanzania, Mkude aliwaambia waandishi wa habari kuwa yeye isingekuwa rahisi kuihama Simba kwani ni timu iliyomtoa mbali kwenye safari yake ya soka.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...