Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAJANGA YANGA, MLIBERIA WAKE ASAKWA ULAYA

WAKATI Yanga ikiwa katika maandalizi ya mwisho kuwavaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jambo jipya limeibuka kuwa yule mshambuliaji wake hatari, Kpah Sherman raia wa Liberia, anatuhumiwa kutoroka kazini nchini Cyprus Kaskazini.


Taarifa kutoka Cyprus Kaskazini barani Ulaya kwa mmoja wa Watanzania wanaoishi nchini humo zimeeleza vyombo vya habari nchini humo, vimeripoti kuwa Mliberia huyo atafunguliwa mashitaka baada ya kutorokea Tanzania.

“Nimesikia huyo mchezaji yuko huko nyumbani, ila huku vyombo vya habari vya hapa vimeripoti timu yake ina mpango wa kufungua kesi Fifa kuelezea kuhusiana na kutoroka kwake,” alisema Mtanzania huyo anayeishi nchini humo.

Juhudi za kuwapata viongozi wa Yanga ilikuwa ni ‘sheedaa’, imeelezwa Mwenyekiti Yusuf Manji yuko nje ya nchi na katibu mkuu mpya, hajaingia ofisini rasmi.

Uongozi wa Klabu ya Centikaya TSK ya Cyprus, umethibitisha kushitushwa na taarifa za Sherman kuondoka nchini humo akidai ana matatizo ya kifamilia.


Lakini baadaye ukapata taarifa kuwa amejiunga na klabu kongwe ya Tanzania iitwayo Yanga nao wakaanza mipango ya kufungua mashitaka kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Akizungumza na Championi Jumatano kutoka Cyprus, Rais wa Centikaya TSK, Meric Erulku amesema ni kweli kumekuwa na hali kutoelewana.

“Kweli hali hiyo imetokea, hatukuambiwa kama anakwenda kwenye majaribio na ruhusa aliyopewa haikuwa ya kwenda kufanya majaribio.

“Kweli tuna mkataba naye, haujaisha na haujavunjwa. Pia hatujalipwa na kulikuwa na mpango wa kwenda Fifa, lakini meneja wake amezungumza nasi.

“Hivyo tunaendelea na hayo mazungumzo ili kujua tutafikia wapi. Kwa kuwa hapa katikati kuna sikukuu, naomba unitafute Jumanne ijayo nitakupa jibu sahihi kama tunakwenda Fifa au tumemalizana nao,” alisema Erulku maarufu kama Buzlat.

Sherman amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Mganda Hamis Kiiza.

Tayari Sherman ameichezea Yanga mechi moja ya kirafiki dhidi ya Simba ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-0.

Hata hivyo, Mliberia huyo ameonekana kukonga nyoyo za mashabiki kiuwezo baada ya mechi hiyo moja.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC