Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Di Maria kukosa mechi ya Liverpool

Angel Di Maria

Mchezaji aliyenunuliwa pesa nyingi zaidi na Manchester United Angel Di Maria atakosa mechi dhidi ya mahasimu hao wao wa jadi Ligi ya Premia Jumapili lakini mzozo wa majeraha Old Trafford kwa sasa unapungua, meneja Louis van Gaal alisema Ijumaa.

Winga huyo wa Argentina, aliyenunuliwa £59.7 milioni kutoka Real Madrid, ambayo ni rekodi Uingereza, atakosa mechi yake ya tatu mfululizo baada yake kukosa kupona jeraha la misuli ya paja.

Mabingwa hao mara 20 wa Uingereza pia watakuwa bila madifenda Luke Shaw na Chris Smalling waliojeruhiwa, sawa na kiungo wa kati Daley Blind.

vLakini meneja wa United Van Gaal alibaki mwenye matumaini Ijumaa, akisema mzozo wake wa majeraha utaisha karibuni. Mzozo huo ulikuwa umemkosesha raha mwanzo wa maisha yake Old Trafford, wakati mwingine akiwa bila wachezaji hadi 12 wakati mmoja. 
 "Sasa ni wachezaji wanne pekee wanaouguza majeraha, hivyo hali ni bora sasa,” Mholanzi huyo aliambia wanahabari.

United wamo nambari tatu kwenye jedwali na alama 28 kutoka kwa mechi 15, alama nane nyuma ya viongozi Chelsea, na wameshinda mechi tano zao za majuzi zaidi. Liverpool wamepitia kipindi kigumu tangu kuanza kwa msimu na wamo nambari tisa, alama saba nyuma ya vijana wa van Gaal.

Kocha huyo wa zamani wa Uholanzi atashuhudia uhasama mkali kati ya klabu hizo mbili kwa mara ya kwanza Jumapili, lakini ameomba ushauri kutoka kwa waliokaa sana klabu hiyo kuelewa vyema uhasama huo.

"Nina Ryan Giggs kama meneja msaidizi na aliwasilisha tathmini yake kuhusu Liverpool na alifanya hivyo vyema sana, nimependezwa sana,” van Gaal alisema kuhusu Giggs aliyechezea klabu hiyo mechi nyingi zaidi.

“Pia tuna mpishi na jina lake ni Mike na ninapokuwa sijui chochote kuhusu uhasama kati ya United na klabu nyingine yeye huniambia. Ni shabiki mkubwa wa Manchester United na kila mara hunijuza.”

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC