Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAXIMO AKIRI KAGERA WALIWAZIDI UJANJA YANGA

Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema kikosi chake kilizidiwa mbinu na Kagera Sugar katika mechi yao ya raundi ya sita ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu ambayo Wanajangwani hao walipoteza kwa bao 1-0 ugenini mjini Bukoba, Kagera juzi.

Kikianza na wachezaji wanne wa kimataifa, Warwanda Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima na Wabrazil Andrey Coutinho na Geilson Santos Santana 'Jaja', kikosi cha Yanga kilijikuta kikipoteza mechi yake ya pili kati ya tatu ugenini baada ya mshambuliaji, Paul Ngwai kuwafungia wenyeji bao kali dakika nane baada ya kuanza kwa kipindi cha pili ikiwa ni mpira wake wa kwanza tangu aingie kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba akitokea benchi.


Akizungumzia mechi hiyo ambayo Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Leiva na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub 'Cannavaro walilambwa kadi nyekundu, Maximo alisema wachezaji wake walizidiwa mbinu na timu hiyo ya Bukoba iliyotumia mbinu ya kupoteza muda, hasa baada ya kupata bao.

"Wapinzani wetu waliharibu mchezo kwa kupoteza muda," alisema Maximo.

Kocha huyo alisema Kagera walipoteza muda makusudi katika mechi hiyo huku pia akiwatupia lawama marefa kwa kuongeza muda 'kiduchu' katika kufidia dakika zilizopotea.
“Walipoteza sana muda, mwamuzi ameona hiyo hali lakini cha ajabu akaongeza dakika tatu tu.

“Haikuwa sahihi na hii si haki hata kidogo. Imenishangaza kwa kweli, ninafikiri mnafurahia kuona Yanga inapoteza,”

aliongeza Maximo ambaye pia alifungwa mabao 2-0 na mchezaji wake wa zamani na kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime katika mechi yao ya kwanza msimu huu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Septemba 20.

Kwa upande wake Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mlage Kabange alisema jana kuwa wanajivunia ubora wa bao lililofungwa na mshambuliaji wao, Ngwai katika mechi hiyo dhidi ya Yanga.

Kabange alisema jana kuwa bao alilofunga Ngwai linawafanya Yanga wasiwe na cha kulalama kwani alifunga goli hilo kiufundi akiifuata krosi ya juu ambayo aliunganisha moja kwa moja na kumuacha Deogratius Munishi 'Dida' asijue la kufanya.

“Ni goli bora kabisa ambalo halina ubishi, magoli kama yale tumezoea kuyaona katika ligi za Ulaya," alisema Kabange.“Hilo litakuwa moja ya mabao bora kabisa na utakubaliana na mimi kama uliliona.

“Tuliyafanyia kazi makosa ya mechi zilizopita (walitoka suluhu dhidi ya Stand United kabla ya kutoka sare ya bao moja dhidi ya Coastal Union), halafu tukawa tayari kwa ajili ya Yanga na kweli umeona soka letu.

“Yanga walicheza vizuri, huenda hawakuwa pia na bahati, lakini hii ilikuwa siku yetu.” alisema zaidi kocha huyo.

Yanga inakamata nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 10 sawa na Azam FC walioko nafasi ya tatu. Nafasi ya kwanza inaendelea kushikiliwa na Mtibwa Sugar wakiwa na pointi 14, tatu mbele ya Coastal Union walioko nafasi ya pili.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC