
Kitimtim cha kutafuta tiketi ya
kuelekea nchini Ufaransa kwaajili ya michuano ya soka barani Ulaya mwaka
2016 iliendelea tena usiku wa kuamkia leo huku nyasi za viwanja kadhaa
zikiwa katika wakati mgumu.
Katika kitimtim hicho timu ya Uholanzi
iliwanyima raha mashabiki wake baada ya kukubali kupokea kipigo cha
mabao 2-0, kutoka kwa Iceland. Nayo Wales ikautumia vema uwanja wake wa
nyumbani baada ya kuigalagaza Cyprus kwa jumla ya mabao 2-1.
Italy
ilikuwa ugenini dhidi ya Malta huku mchezo huo ukimalizika kwa kila
timu kucheza pungufu baada ya wachezaji wao kuoneshwa kadi nyekundu.
Michael
Misfud wa Malta alikuwa wa kwanza kwenda nje katika dakika ya 27 huku
Leonardo Bonucci wa Italy akifuatia katika dakika ya 73 ya mchezo, hadi
mwisho wa kipute hicho Italy ikawabanjua wapinzani wao bao 1-0.