Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI YA WATANZANIA

Vijana wa Taifa Stars wamemshusha pumzi kocha wa timu hiyo, Mart Nooij baada ya kuichapa Benin mabao 4-1 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jana.

Mabao ya Stars yalifungwa na Nadir Haroub kwa kichwa dakika ya 16 akiunganisha vizuri mpira wa faulo uliopigwa na Erasto Nyoni na Amri Kiemba alifunga kiufundi bao la pili dakika ya 40 akitumia makosa ya beki wa Benin, Ore Fortune kabla ya Thomas Ulimwengu hajafunga la tatu katika dakika ya 49 akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa na bao la nne lilifungwa na Juma Liuzio dakika ya 71 akitumia vizuri pasi ya Ulimwengu.

Benin ilipata bao lake pekee katika dakika ya 90 lililofungwa na Suanon Fadel kwa shuti akitumia vizuri pasi ya Stephane Sessegnon aliyewatoka mabeki wa Stars.


Katika mechi mbili zilizopita, Taifa Stars ilichapwa na Burundi 2-0 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa, pia ilichapwa na Msumbiji 2-1 katika mechi ya kuwania kufuzu kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2015.

Katika mechi ya jana, Stars ilicheza soka ya kasi na pasi nyingi wakati Benin ilikuwa ikijilinda zaidi na kucheza pasi nyingi huku wachezaji wake wakivizia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Pia Stars ilikuwa imara katika safu ya kiungo kilichokuwa chini ya Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba na kuwakabili vyema viungo wa Benin wakiongozwa na Sessegnon anayechezea West Bromwich ya England na Adeoti Jordan.

Benin ilikubali kufungwa mabao mawili katika kipindi cha kwanza. Ilipofungwa bao la kwanza, ilimka na kutafuta bao la kusawazisha, hivyo kuipa mwanya Taifa Stars kupata bao la pili.

Kipindi cha pili Benin ilianza kwa kumtoa kipa Farnoue Fabien na nafasi yake kuchukuliwa na Allagbe Saturnin.

Mabadiliko hayo hayakuizuia Stars kufunga kwani ilipata bao la tatu na kuendelea kutawala huku Benin ikijilinda na kuendelea kushambulia kwa kushtukiza.

Baada ya kufungwa bao hilo la tatu, ilifanya mabadiliko kwa kuwaingiza Baraze Seidou na Adadou Mohamed huku Dossou Jodel na Mama Seibou wakitoka. Pia iliwaingiza Sossa Didier, Dalmeida Sessy na Suanon Fadel na kuwatoa Djigla David, Ore Fortune na Tossavi Erick.

Taifa Stars nayo ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Ngassa, Kiemba, Nadir Haroub, Harun Chanongo na Ulimwengu na nafasi zao zilichukuliwa na Juma Luizio, Said Morad, Said Ndemla na Mcha Khamis.

Timu zote zilinufaika kwa mabadiliko hayo Stars kwani ilipata bao la nne na Benin ilipata bao la kufutia machozi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...