Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SIMBA YAPATA PIGO SOUTH AFRICA

Klabu ya Simba imepata pigo jingine kabla ya kukutana na wapinzani wao wa jadi Yanga baada ya kipa wao Hussein Sharrif ‘Casillas’ kuumia ugoko katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Orlando Pirates nchini Afrika Kusini walipoweka kambi.

Hiyo ni habari mbaya kwa Simba ambayo kipa wake namba moja Ivo Mapunda hayupo fiti kwa asilimia 100 kutokana na majeraha ya kidole ambayo aliumia kwenye mazoezi ya klabu hiyo visiwani Zanzibar hivi karibuni.


Casillas kupitia mtandao wake wa kijamii aliandika kusikitishwa kwake kukosa mechi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga itakayochezwa Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Taifa kwa sababu ameumia.

Rais wa Simba, Evans Aveva alithibitisha kuumia kwa Casillas juzi na jana walikuwa wanahangaikia matibabu yake.

“Ni kweli ameumia, lakini mpaka sasa hatujajua atachukua muda gani nje ya uwanja, ni pigo kubwa kwetu lazima nikiri hilo,” alisema Aveva.

Casillas na Manyika Peter ni makipa waliosajiliwa na Simba wakati wa majira ya kiangazi mwaka huu baada ya Simba kuachana na kipa Mghana Yaw Berko na kubaki na Mapunda.

Wachezaji majeruhi wamezidi kuongezeka Simba, kwani pia Mkenya Raphael Kiongera aliumia katika mechi dhidi ya Coastal Union.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...