Ruka hadi kwenye maudhui makuu

PHIRI ATAMBIA REKODI KUIFUNGA YANGA

Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, amesema rekodi yake nzuri katika mechi dhidi ya watani wa jadi ndiyo 'itakayowamaliza' wapinzani wao Yanga katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo itafanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba iko jijini Johannesburg, Afrika Kusini kujiandaa na mchezo huo ambao huvuta hisia za mashabiki wa soka ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili, Phiri ambaye katika misimu miwili tofauti aliyoinoa Simba kabla ya huu amefungwa mara moja tu na Yanga, alisema kambi ya Simba huko Afrika Kusini haiangalii mechi moja dhidi ya watani hao wa jadi, ila ni maalumu kurejesha morali kwa wachezaji msimu huu na haifikirii timu hiyo peke yake.


Phiri alisema amefurahishwa na maamuzi yaliyofanywa na viongozi wa klabu hiyo kuipeleka timu Afrika Kusini kujiandaa na kujipima na klabu za huko hali inayowapa wachezaji nafasi ya kupata uzoefu na mbinu mpya za kuwakabili washindani wake.

"Ni nafasi pekee na adimu kwa timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kupeleka timu zao Afrika Kusini kujiandaa, wengi huogopa gharama lakini matokeo mazuri yanatokana na kuwekeza," alisema Phiri.

Kocha huyo alisema kuwa anaamini matokeo ya kambi hiyo yatapatikana na si kwa kuangalia mechi hiyo ya Jumamosi peke yake.

"Nimekuta ligi ina changamoto tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma, nimejifunza na nitaendelea kujifunza ili kukiboresha kikosi, tunamatumaini ya kufanya vizuri mechi zinazofuata," aliongeza Phiri.

Kuhusiana na suala na nani atadaka katika mechi ya Jumamosi kutokana na makipa wake, Ivo Mapunda (alikuwa majeruhi) na Hussein Shariff 'Casillas' naye kuumia, litajulikana Ijumaa jioni.

Phiri jana alizuia timu hiyo kucheza mechi ya kirafiki na badala yake leo ndiyo itashuka kuikabili Jomo Cosmos.

CASILLAS NJE WIKI SITA

Kipa Hussein Shariff 'Casillas' ataikosa mechi dhidi ya Yanga itakayofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa kutokana na kuwa nje kwa muda wa wiki sita, imefahamika.
Casillas ambaye ametua Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro aliumia mguu Jumamosi wakati timu hiyo ikicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Orlando Pirates inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka ya Afrika Kusini.

Habari zilizopatikana jana kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa kipa huyo alifanyiwa operesheni ya mguu juzi Jumatatu katika hospitali mojawapo jijini Johannesburg na jana ndiyo alitarajiwa kutoka hospitali.

Taarifa zaidi kutoka katika kambi ya Simba zinaeleza kwamba, baada ya Casillas kuumia, benchi la ufundi pamoja na viongozi wa timu hiyo 'walichanganyikiwa' kutokana na kuiwaza mechi ya Jumamosi.

"Casillas alilazwa na amefanyiwa operesheni, atakuwa nje kwa muda wa wiki sita," alisema kiongozi mmoja wa Simba.

Aliongeza kuwa hali ya kipa chaguo la kwanza la timu hiyo, Ivo Mapunda, ambaye naye alivunjika kidole bado hajapona hivyo sasa wameanza kumuandaa kipa namba tatu na chipukizi, Peter Manyika 'Junior'.

"Viongozi wengine wamekuja jana (juzi) usiku wamezungumza sana na wachezaji, hiyo ndiyo hali halisi," aliongeza kiongozi huyo.

Tayari Wekundu wa Msimbazi wameshacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa ambapo ya kwanza walitoka sare ya bila kufungana na Orlando Pirates huku Bidvest Wits University ikiwachapa mabao 4-2.

Wapinzani wao Yanga wenyewe wameweka kambi jijini. Simba itashuka uwanjani ikiwa na pointi tatu mkononi wakati Yanga yenyewe ina pointi sita huku vinara wa ligi hiyo Mtibwa Sugar wakitanua kileleni kwa pointi tisa.

'FRIEND'S' WATUA SAUZI

Viongozi wa Kundi la Friends of Simba wakiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Kassim Dewji 'KD' walitua Johannesburg juzi asubuhi ili kukutana na wachezaji wa timu hiyo.

Taarifa kutoka ndani ya kambi hiyo zinaeleza kuwa 'ujio' wa viongozi hao ni kutaka kuzungumza na wachezaji na kuwapa jukumu la kuhakikisha wanapambana na kushinda Jumamosi.

Chanzo cha gazeti hili kilisema kuwa mbali na mazoezi, wachezaji wamekuwa wakipelekwa matembezi ili waondoe mawazo ya kuiogopa Yanga na kuiona mechi hiyo ni ya kawaida lakini wakitakiwa kushinda ili kuipa klabu heshima.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC